Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa timu hiyuo, Rogasian Kaijage amesema, juhudi zinazofanywa na Shirikisho la soka Nchini TFF inajitahidi na vitu vingine TFF inashindwa kwa sababu inakosa fedha.
Kaijage amesema, Twiga Stars ndiyo timu pekee iliyojihakikishia kushiriki michuano ya All African Games ambapo timu zingine bado haijajulikana, hivyo inatakiwa serikali na watu binafsi kujitokeza kwa hali na mali ili kuiwezesha timu hiyo kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo.

