Tuesday , 24th Jun , 2014

Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa Miaka 17 (Serengeti Boys) imeingia kambini leo kujiandaa na mechi ya kuwania kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika mwakani nchini Niger dhidi ya Afrika Kusini.

Kikosi cha Serengeti Boys

Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa Miaka 17 (Serengeti Boys) imeingia kambini leo kujiandaa na mechi ya kuwania kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana zitakazofanyika mwakani nchini Niger dhidi ya Afrika Kusini mchezo utakaopigwa Julai 28 mwaka huu katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Boniface Wambura amesema timu hiyo ipo chini ya Kocha Abuu Omary na atakuwa na timu hiyo kwa muda wa majuma mawili na baada ya hapo atafanya mchujo kwa ajili ya kupata wachezaji 25 watakaocheza mechi hiyo.

Wambura amesema Kocha huyo aliyekuwa akifundisha kikosi cha vijana chini ya miaka 20 cha Zanzibar atafanya kazi na mshauri wa Ufundi Stewart Hall mpaka muda ataokaopatikana kocha msaidizi wa kikosi hicho