Sunday , 27th Jan , 2019

Kama umekuwa ukimfuatilia vizuri msanii wa Hip Hop, Young Killer, utagundua kuwa ni mshambiki wa klabu gani hapa nchini kutokana na namna anavyotumia mashairi yake kuisapoti.

Young Killer

Young Killer ni shabiki mkubwa wa Yanga na katika nyimbo zake nyingi amekuwa akiitaja sana na mwenyewe akikiri kuwa kitu pekee anachokipenda tofauti na mziki wake ni soka, kwa maana ya kucheza na kutazama pia.

Katika wimbo wake aliouachia mwishoni mwa mwaka uliopita wa 'Sinaga Swagga III' ametumia mashairi yake akiifananisha Yanga na Barcelona au Arsenal, huku Simba akiilinganisha na Mbao FC ambazo leo hii zimekutana katika uwanja wa taifa katika mchezo a kuwania nafasi ya tatu ya mashindano ya SportPesa.

Moja ya mstari kwenye wimbo huo, Young Killer amesema, "sasa hivi Simba na Mbao ndio washindani, ila Barcelona, Arsenal ndiyo level za jangawani ( Young Africans)".

Mashabiki wa Simba wameonesha kutoridhishwa na kiwango cha timu yao katika michuano hiyo huku wengi wao wakikasirishwa na klabu hiyo kuondolewa hatua ya nusu fainali wakati walikuwa wakiamini kuwa wana nafasi kubwa ya kushinda kombe hilo.

Simba imeibuka na ushindi wa nafasi ya tatu wa michuano hiyo kwa kuifunga Mbao FC kwa mikwaju ya penalti 5-3 baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana, ambapo sasa itazawadiwa kiasi cha Dola 7500 za kimarekani.