
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Genk, Mbwana Samatta.
KRC Genk ina nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya makundi baada ya kushinda mchezo wa kwanza katika uwanja wake wa nyumbani kwa mabao 5-2, mchezo ambao Samatta alifunga hat-trick yake ya kwanza kwa klabu yake.
Nahodha huyo wa Taifa Stars ataipigania klabu yake kurejea michuano ya Europa League tangu msimu wa 2016/17, msimu ambao Mbawana Samatta alisajiliwa na klabu hiyo kutokea TP Mazembe ya jamhuri ya kidemocrasia ya Congo.
Katika msimu wao wa mwisho kushiriki Europa League, Genk iliishia hatua ya robo fainali baada ya kutolewa na Celta Vigo ya Hispania kwa uwiano wa magoli 4-3 katika mechi zote mbili, kiwango cha ufungaji alichonacho mshambuliaji huyo kwa sasa kitakuwa msaada mkubwa katika mchezo huo kwani ameshafunga mabao nane katika mechi tano za karibuni alizocheza.
Baada ya mchezo huo, Samatta anatarajiwa kuwasili katika kambi ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ inayojiandaa na mchezo wa kufuzu michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Uganda utakaopigwa, 8 Septemba mjini Kampala nchini humo.