Tuesday , 24th May , 2016

Ratiba ya fungua dimba ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF) imetoka ambapo wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo Yanga wanataraji kuanzia ugenini kwa kuvaana na Warabu wa Algeria.

Ratiba ya michezo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika makundi A na B.

Yanga SC itafungua dimba na Mouloudia Olympique Bejaia nchini Algeria Juni 17, mwaka huu katika Kundi A Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Siku hiyo hiyo , mabingwa wa zamani wa klabu bingwa barani Afrika, TP Mazembe ya DRC watakuwa wenyeji wa Medeama ya Ghana katika mchezo mwingine wa kundi hilo.

Mechi za Kundi B siku hiyo; ni kati ya Kawkab Marakech watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi Etoile du Sahel katika mchezo wa Kundi B nchini Morocco, wakati F.U.S Rabat watakuwa wenyeji wa Ahly Tripoli nchini Morocco pia.

Ikitoka Algeria, Yanga itarejea nyumbani katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kuikaribisha TP Mazembe Juni 28, kabla ya kumaliza na Medeama ya Ghana Julai 15,jijini Dar es Salaam pia.

TP Mazembe ndiyo timu ambayo anachezea Mtanzania Thomas Ulimwengu ambaye naye atarejea nchini kwa mara ya kwanza akiwa na timu hiyo kucheza na Yanga ambayo hajawahi kukutana nayo hata mara moja tangu aanze kucheza soka la ushindani mshambuliaji huyo wa taifa stars akijulikana zaidi kwa juna la Rambo na mashabiki wa soka nchini Congo DR.

Na hii ni ratiba kamili kama inavyoonekana chini.

RATIBA KOMBE LA SHIRIKISHO

KUNDI A:

Juni 17, 2016

MO Bejaia Vs Yanga SC

TP Mazembe Vs Medeama

Juni 28, 2016

Yanga SC vs TP Mazembe

Medeama Vs MO Bejaia

KUNDI B:

Kawkab Marrakech Vs Etoile du Sahel

F.U.S Rabat Vs Ahly Tripoli

Juni 28, 2016

Etoile du Sahel Vs F.U.S Rabat

Ahly Tripoli Vs Kawkab Marrakech