Sunday , 2nd Sep , 2018

Katika kuboresha soka la wanawake nchini,Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema wanafanya mipango ya kuitafutia mechi kubwa timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ili iweze kupata uzoefu zaidi.

Kikosi cha Twiga Stars

Akitoa pongezi zake kwa Twiga Stars ambao wametoka kutwaa ubingwa wa Jumuiya ya Africa Mashariki nchini Burundi, Karia ameweka wazi kuwa timu hiyo imeimarika vya kutosha kilichobaki ni kupata uzoefu wa kucheza na mataifa makubwa kisoka.

"Tunawapongeza sana Twiga Stars kwa mafanikio haya, kama shirikisho tunafanya mpango wa kutafuta mechi za kirafiki na mataifa yenye ushindani katika soka la wanaake ili kuimarisha kikosi hiki kwaajili ya mashindano makubwa ikiwemo AFCON'' Alisema jana.

Mbali na pongezi hizo Karia amewataka wachezaji hao kulinda nidhamu ambayo wamekuwa wakiionesha kwenye timu ya taifa pia wawe hivyo hivyo kwenye vilabu vyao.

Kwasasa wachezaji wa kikosi cha Twiga Stars wameruhusiwa kurudi kwenye timu zao mpaka watakapoitwa tena kwaajili maandalizi ya mechi mbalimbali za kirafiki na mashindano.