Sunday , 16th Mar , 2014

SMG kumwashia moto Mrusi PTA

Pambano la masumbwi yakulipwa la uzito wa kilo 81 light heavy baina ya bondia mtanzania Francis Cheka smg na bondia mrusi Valery Brudov sasa litafanyika tarehe 5 mwezi wa nne likiwa chini ya usimamizi wa TPBF

Awali pambano hilo lilikua chini ya promota Jay Msangi wa holofame promotions na sasa litakua chini ya uratibu wa kampuni mpya ya Mawenzi International Focus limited chini ya uongozi wa Musa Kova

Kubwa zaidi baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo kwa wahusika wa pambano hilo,mmoja wa wadhamini wa maandalizi ya bondia Francis cheka kampuni ya Bitebo hair designing chini ya Abdalah Bitebo wameahidi kumpeleka Cheka nje ya nchini kufanya maandalizi ya mpambano huo.