
Akizungumza na East Africa Radio, kocha wa timu hiyo, Mbwana Makata amesema, kambi hiyo imeanza leo ambapo watakuwa wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo.
Makata amesema, mchezo huo ni muhimu kwao kuhakikisha wanapata ushindi ili kujihakikishia wanabaki kwenye ligi kuu soka Tanzania Bara kutokana na nafasi mbaya waliopo hivi sasa.
Prisons inahitaji ushindi katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Mei tisa uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ili kujinasua mkiani na kukwepa kushuka daraja kutokana na timu nyingi kufungana na pointi 28.