Patrick Patrick akiwasili Uwanja wa Ndege jijini DSM
Mamia ya mashabiki wa klabu ya Simba ya jijini DSM, mchana wa leo, wamejitokeza kumlaki kocha wao mpya Mzambia Patrick Phiri alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kocha huyo ambaye hii itakuwa ni mara yake ya Tatu kuifundisha klabu hiyo, amewasili milango ya saa Saba na dakika 20 mchana wa leo na moja kwa moja kuzikabili kamera na vinasa sauti vya waandishi wa habari wakiwemo wa EATV.
katika mahojiano hayo, Phiri ameahidi kurejesha makombe yalipotea kwa kipindi kirefu Msimbazi.
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo bwana Collin Frisch ambaye ndiye aliyempokea kocha huyo kwa niaba ya klabu, alisita kuzungumzia mkataba wa kocha huyo na kama amekuja moja kwa moja au ataondoka halafu ndio aje moja kwa moja.
Patrick Phiri amekuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Zdravko Logarusic wa Croatia aliyetimuliwa mwishoni mwa juma. Patrick Phiri aliifundisha Simba kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka 2003 mpaka 2005 na baadaye 2008 mpaka 2010.