
Manny Pacquiao
Mabondia hao ni Amir Khan na Kell Brook, wa Uingereza, Jeff Horn wa Australia na Terence Crawford, wa Marekani.
Pacquiao amesema pambano hilo la kutetea mkanda ambao alishinda katika mwezi wa Novemba mwaka uliopita, litafanyika katika nchi za falme za kiarabu.
Mfilipino huyo mwenye umri wa miaka 38, na bingwa mara 6 wa dunia, alitangaza kustaafu katika mwezi wa Aprili, mwaka uliopita, lakini alirejea tena ulingoni na kumshinda Jessie Vargas mwezi wa Novemba, mwaka jana.