Thursday , 21st Jan , 2016

Kocha mkuu wa vinara wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger anaamini atapata huduma za nyota wake Mesut Ozil na Alexis Sanchez kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Chelsea itakayopigwa siku ya jumapili.

Kiungo mchezeshaji wa Arsenal Mesut Ozil(kulia)na mshambuliaji Alexis Sanchez(kulia)katika picha wanatarajiwa kuikabili Chelsea siku jumapili.

Wenger ambaye amekua na msimu mzuri msimu huu amesema hali ya majeruhi hao wote wawili ni ya kuridhisha na anapata matumaini watacheza kwenye mechi hiyo .

Ozil alikuwa anauguza jeraha la kidole cha mguu hali iliyopelekea kukosa mechi iliyopita dhidi ya Stoke City iliyomalizika kwa sare ya 0-0 huku Sanchez akikosekana kwenye kikosi cha Arsenal tangu novemba mwaka jana kutokana na maumivu ya misuli ya paja.

Katika hatua nyingine Wenger amesema kiungo Francis Coquelin na mshambuliaji Dany Weklbaeck wote wameanza kufanya mazoezi mepesi huku wakionyesha maendeleo mazuri ya kupona majeraha yaliyokua yakiwakabili.

Kuhusu mchezo husika kocha huyo amesema mechi itakua ngumu licha ya Chelsea kutokua na matokeo mazuri lakini wana wachezaji wenye ubora ambao wanaweza kuwapa wakati mgumu kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Emirate.