Friday , 15th Jan , 2016

kiungo mchezeshaji wa klabu ya soka ya Arsenal Mesut Ozil ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ujerumani kwa mara ya nne ndani ya miaka mitano iliyopita.

Kiungo mchezeshaji wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ujerumani Mesut Ozil akiwa dimbani kwenye mechi za ligi kuu nchini Uingereza

Ozil ambaye kwa sasa ndiye kinara wa pasi za mwisho katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza amepigiwa kura 51000 na msahabiki zilizompa asilimia 45.9 na kuwapiku Thomas Muller wa Bayern Munich aliyepata asilimia 15.9 na Jonas Hector aliyepata asilimia 13.5 ya kura zote.

Nyota huyo alipoteza tuzo hiyo kwa kiungo wa Real Madrid Toni Kroos mwaka 2014 baada ya kuitwaa miaka mitatu mfululizo.

Akiwa na Arsenal msimu huu amepiga pasi za magoli 16 na kutengeneza nafasi 87 na kumfanya kinara kwa kuwapiku nyota wa ligi zote tano bora barani Ulaya.