Friday , 8th Jun , 2018

Baada ya tetesi kwamba Deus Kaseke huenda akaungana na kocha Hans Van Pluijm pamoja na Tafadzwa Kutinyu kutoka Singida United kujiunga Azam, Mkurugenzi wa Singida United amesema Kaseke atatimkia Afrika ya Kusini ambako amepata ofa.

Festo Sanga amekanusha taarifa za muda mrefu ambazo zimekuwa zikimuhusisha Kaseke kujiunga na Azam kutokana na uhusiano wake mzuri na Hans van Pluijm ambaye ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

“Deus Kaseke amepata ofa kutoka Afrika Kusini, kuna timu imepanda ligi kuu ya huko inamuhitaji Kaseke. Sina taarifa kwamba anakwenda kuungana na kocha Hans”, amesema Sanga.

Sanga ameongeza kuwa wachezaji wengine watano wanaotarajia kuondoka klabuni hapo baada ya kupata ofa mbalimbali ndani na nje ya nchi.