Baadhi ya wachezaji wa Ngorongoro Heroes wakishangilia baada ya kuiondoa Kenya mashindanoni
Maandalizi ya mechi ya kimataifa ya kuwania tiketi yakucheza michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 itakayochezwa kesho katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baina ya timu ya taifa ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) dhidi ya timu ya Nigeria (Flying Eagles) yamekamilika.
Makocha wa timu hizo leo wamezungumzia mechi hiyo ambapo kocha wa Ngorongoro Heroes John Simkoko na nahodha wa timu hiyo Aishi Manula wamesema wako tayari kwaajili ya mchezo huo japo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu ya Nigeria
Kwa upande wa Nigeria [flying Eagles] kupitia kwa kocha msaidizi wa timu hiyo Nduka Obadi amesema hawaijui vizuri timu ya Ngorongoro heroes lakini wao wamejipanga kucheza vizuri na kupata matokeo