Ngassa ambaye jana alifanya mazoezi na timu yake ya zamani, Yanga SC Uwanja wa Karume, Dar es Salaam alipewa ruhusa ya kuja kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars.
Bahati mbaya, Ngassa aliondolewa katika kambi Stars iliyokuwa inajiandaa kwa mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda Raundi ya Kwanza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kusema haruhusiwi kucheza kwa kuwa amekwishasaini Mkataba na timu ya Afrika Kusini, japokuwa hajaanza kuitumikia.

