Akiongea kwenye sherehe za utoaji tuzo za waandishi wa habari za michezo nchini humo Tebas amesema, ''Neymar ni mchezaji mkubwa, natamani nimuone tena akicheza La Liga ila kuhusu timu atakayocheza sitaki kujua''.
Neymar ambaye alisajiliwa na PSG kutoka Barcelona Juni 2017 hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao 26 kwenye mechi 24 alizoichezea timu hiyo.

Kwa upande mwingine bosi huyo wa La Liga amewahakikishia wanahabari kuwa msimu ujao wa ligi 2018/19 hakutakuwa na matatizo ya uamzi kwenye baadhi ya matukio kwasababu teknolojia ya VAR itaanza kutumika nchini humo.

