Thursday , 21st Jan , 2016

klabu ya soka ya Barcelona imeanza vyema Robo Fainali ya Kombe la Mfalme huku Atletico Madrid wakibanwa katika Mechi za Kwanza za hatua hiyo hapo Jana.

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao katika mchezo wa jana dhidi ya Athletic Bilbao

Wakiwa ugenini katika uwanja wa San Mames, Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey, Barcelona, walishinda Ugenini Bao 2-1 kwa kuwachapa Athletic Bilbao kwa mabao ya Munir El Haddad na Neymar katika Dakika za 18 na 24 na bao pekee la Bilbao likifungwa na Artulo Arduliz

Huko Estadio Municipal de Balaidos Celta Vigo waliwabana Atletico Madrid na kutoka nao 0-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya Copa del Rey.

Hii leo usiku mechi mbili za kwanza za robo fainali zitapigwa ambapo Valencia wataikaribisha Las Palmas nayo Sevilla FC itapambana na CD Mirandes huku mechi za marudiano zikitarajiwa kuchezwa januari 27 mwaka huu.