
Shime amesema, atahakikisha anasajili wachezaji atakaoridhika na viwango vyao tofauti na ambao wako katika kikosi chake kwa sasa.
Shime amesema, kikosi chake kwa sasa kipo kambini kikijiwinda na mchezo wao wa mzunguko wa 10 dhidi ya Yanga utakaofanyika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mgambo Shooting inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikiwa na Pointi 11 sawa na Majimaji ya mjini Songea lakini zikitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.