
Bodi ya ligi Tanzania TPL Board imewataka waamuzi watakaochezesha michezo miwili ya mwisho ya ligi daraja la kwanza toka kundi C kufuata sheria 17 za soka, ili kuzuia malalamiko ya aina yoyote kutokana na maamuzi ya mechi hizo ,ambazo ndizo zitatoa timu moja, itakayounganana timu za Polisi morogoro na Ndanda ya Mtwara, ambazo tayari zimepanda ligi kuu Tanzania bara mapema .
Mtendaji mkuu wa Bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema kuwa kutokana na hali ilivyo ni wazi mkoa wa Shinyanga mwakani utakua na timu ya ligi kuu kwakua kesho ndio kama fainali kwa timu mbili za Mwadui FC na Stand united za Shinyanga ambazo zitakua viwanjani katika viwanja tofauti zikiwania nafasi hiyo adimu
Mwadui ambayo kesho itakua mjini Dodoma kuvaana na Polisi ya huko inaongoza kundi C ikiwa na pointi 28 ikifuatiwa na timu ya Stand united yenye Pointi 26 huku kesho nayo ikiwakaribisha Toto Africans ya Mwanza katika uwanja wa Kambarage, katika kundi C hakuna timu nyingine yeyote inayoweza kufikia pointi za timu hizo mbili za Shinyanga.
