Akiongea mapema leo kwenye kipindi cha 'Shabiki On Saturday' kinachoruka kupitia East Africa Television, Mwana FA ameweka wazi hilo akiamini msimu huu Simba watachukua ubingwa msimu huu.
''Mimi nimeongea na mashabiki wenzangu wa Simba akiwemo Mo Dewji kuwa sitashangilia ubingwa wa Simba msimu huu endapo hatutaifunga Yanga kesho kwasababu uwezo tunao,'' amesema.
Kwa upande mwingine Mwana FA amesema anaamini Simba ina kikosi bora msimu huu ambacho kitasaidia kumaliza ukame wa taji la ligi kuu ndani ya klabu hiyo uliodumu kwa misimu mitatu.
''Ubingwa msimu huu uko wazi ukiangalia alama za Simba ni 59 ina maana Yanga hata akishinda viporo vyake viwili bado hawezi kuzifikia kwasababu ana alama 48 ataishia 56 tu hivyo ni wazi ukame wa mataji msimu huu unaisha,'' ameongeza.