Mwamuzi Ahmada Simba (mwenye nguo ya njano katikati) akisuhisha jambo wakati wa mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting katika dimba la Taifa DSM
Hatua hii imefikiwa baada ya utetezi wa Mwamuzi Simba kudai kwamba hakuona tukio la Mchezaji wa Young African, Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa na kumwonya mchezaji kwa kadi njano.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo ambao Young Africans walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka huu.
Kadi hiyo ya njano ilikuwa ni ya kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.
Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.

