Akiongea kwenye mahojiano na East Africa Television Mwalimu amesema moja ya mipango yake mikubwa ni kuisaidia timu hiyo isiende kuwa mshiriki bali ikawe mshindani.
''Mimi ni mwanamichezo na bahati nzuri Kinondoni tumeingiza timu ligi kuu na imenifanya niwe na shauku ya kuwa Mbunge ili nitumie talanta zangu zote kuisaidia timu hiyo kwasababu michezo ni sehemu ya maisha yangu'', amesema.
KMC imepanda ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya kuibuka kinara wa kundi B kwenye ligi daraja la kwanza kwa kuwa na alama 28, hivyo msimu wa 2018/19 itakuwa miongoni mwa timu 20 za ligi hiyo.

