Saturday , 12th Apr , 2014

Siku chache baada ya timu ya Stand United ya Shinyanga kutangazwa kupanda daraja kucheza ligi kuu ya soka ya Tanzania bara msimu ujao, Kocha wa klabu ya Mwadui, Jamhuri kihwelu "Julio" amekata rufaa kupinga kupanda kwa timu hiyo.

Kocha wa timu ya Mwadui Jamhuri Kihwelu

Siku chache baada ya timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga kutangazwa kupanda daraja kucheza ligi kuu ya soka ya Tanzania bara msimu ujao, Kocha wa klabu ya Mwadui, Jamhuri Kihwelo "Julio" Perreira Albeto Talantin amekata rufaa kupinga kupanda kwa timu ya Stand United.

Kocha Julio amesema kupanda kwa timu ya Stand United ni kutokana na mipango iliyofanywa na Shirikisho la kandanda nchini TFF wakishirikiana na baadhi wa viongozi wa kisiasa na kupelekea wao kupokwa pointi katika moja ya michezo yao waliyoshinda hali inayochangia TFF kushindwa kuitangaza timu hiyo bayana na atafanya kila awezalo ili kuipata haki ya timu yake.

Julio amesema anaendelea kufanya usajili kwani anaamini timu yake ndiyo bingwa katika kundi lake lililokuwa na timu za Toto Africans ya Mwanza, Kanembwa United, Polisi Dodoma, Stand United na Mwadui Spors Club.