Friday , 15th Jan , 2016

Mchezaji wa tenisi namba moja nchini Uingereza Andy Murray atafungua dimba la michuano ya wazi ya Australia januari 18 atakapoumana na Mjerumani Alexander Zverev.

mashindano ya wazi ya Australia

Katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza Murray atakuwa akiwania kushinda ili asonge mbele zaidi akiwania ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kupoteza katika fainali nne zilizopita ikiwemo ya mwaka jana dhidi ya Novan Djokovic.

Kwa upande wake bingwa mtetezi ambaye pia ndiye kinara kwa ubora duniani Mserbia Novan Djokovic ataumana na mchezaji waia wa korea kusini Hyeon Chung katika mechi yake ya kwanza.

Kwa upande wa wanadada bingwa mtetezi wa michuano hiyo Serena Williams amepangwa kwenye kundi gumu ambapo ataanza kampeni za kutetea taji lake dhidi ya muitalia Camila Giorgi.