Tuesday , 5th Jan , 2016

Timu ya Mtibwa Sugar imeisukuma nje ya mashindano ya Mapinduzi timu ya Mafunzo ya visiwani Zanzibar baada ya kuifunga kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa leo kwenye uwanja wa Amaan.

Kikosi cha wakatmiwa wa Mtibwa Sugar katika picha ya pamoja kikijiandaa kwa moja ya mechi za ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Said Bahanuzi ndiye aliyeitupa nje Mafunzo kwani goli lake la dakika ya 12 kipindi cha kwanza lilidumu mpaka dakika zote 90 za mchezo zinamalizika.
Ushindi huo unaipa matumaini Mtibwa Sugar kwasababu imefikisha pointi nne baada ya michezo miwili na kubakiza mchezo mmoja ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba itakapocheza dhidi ya Azam FC.
Matokeo ya leo ni faraja kwa Mtibwa ambao goli lao la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Azam lilikataliwa na mwamuzi wa pembeni Dalila Jaffar Mtwana ambaye tayari ameshawajibishwa kwa kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi wanaoendelea kuchezesha mashindano hayo.