Mourinho amelazimika kueleza hayo baada ya kuwepo kwa utata kwenye mchezo wa jana usiku wa kombe la FA dhidi ya Huddersfield ambapo Man United ilizuiliwa bao muda mchache kabla ya mapumziko kwa kutumia teknolojia hiyo.
Sina tatizo na VAR naiunga mkono lakini lazima tuwe makini sana na maamuzi mengine tuyaache kwa mwamuzi na anaweza kuwa na maamuzi sahihi juu ya tukio kutokana na sheria inavyosema kwasababu sio kila mtu anapozidi ni ''Offside'', amesema Mourinho.

Moja ya matukio ambayo yalikuwa nguzo kwenye mchezo wa jana ni lile goli la Juan Matta ambalo lilikataliwa kuwa alikuwa amezidi huku refarii akiamini kuwa hakuwa amezidi lakini VAR ikathibitisha kuwa sio goli.
Aidha Mourinho amesema VAR inahitajika sana kwenye baadhi ya matukio na ni muhimu kutumika lakini lazima iangaliwe vizuri kama mwamuzi ametafsiri vizuri sheria.


