Jose Mourinho
Mourinho, ambaye alifutwa kazi mara mbili na Chelsea, aliitwa 'Yuda' na mashabiki wakati wa mechi hiyo, iliyokuwa na kandanda safi kwa timu zote mbili kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Hata hivyo, aliwajibu kwa kuwaelekezea vidole vitatu, ishara ya mataji matatu ya ligi aliyoyashinda akiwa na klabu hiyo.
Alisema baadaye: "Hadi wampate meneja ambaye atawashindia mataji manne ya Ligi ya Premia, mimi bado ni nambari moja. Hadi wakati huo, Yuda ndiye nambari moja."
Bao la ushindi la Chelsea katika mechi hiyo ya Jumatatu lilifungwa na N'Golo Kante katika dakika ya 51, huku United wakimaliza na wachezaji 10 baada ya Ander Herrera kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 35.

