
Mourinho amesema ubora na matokeo mazuri ya Manchester City haimanishi kuwa timu zingine hazina uwezo bali timu hiyo inajitahidi wapinzani wasiifikie hivyo wao kama Man United wanajitahidi kuhakikisha wanabaki katika nafasi ya pili.
"Tuko katika nafasi hii karibu msimu wote huu, tulikuwa wa kwanza kwa wiki chache lakini muda mwingi tumekuwa katika nafasi ya pili, nadhani hatutafika katika nafasi za tatu, nne, tano au sita, kitu ambacho ni bora kuliko msimu uliopita'', amesema.
Mourinho amesema timu zingine kama Chelsea ambaye ni bingwa mtetezi inajitahidi na imefanya usajili mzuri huku Liverpool akisema ni timu kubwa. Arsenal amesema imefanya vizuri kwenye usajili pamoja na Tottenham kuwa ni timu bora na inawakimbiza hivyo wanajitahidi kuhakikisha haziwafiki.
Mourinho amesisitiza kuwa tofauti ya Manchester City na timu zingine ni kuwa timu hiyo inafanya vizuri sana msimu huu na sio kwamba timu zingine hazina ubora kama wanavyosema baadhi ya watu. Man U ipo nafasi ya pili na alama 53 nyuma ya Man City yenye alama 68.