
Mkwasa amesema, licha ya kuwa na baadhi ya wachezaji wenye matatizo madogomadogo lakini hayawazuii kuweza kuliwakilisha taifa hapo kesho na kuweza kupata matokeo mazuri.
Mkwas aamesema, atajaribu kuweka kikosi imara zaidi chenye mlengo wa kimashambulizi zaidi kwani mchezo huo ni muhimu na wanahitaji matokeo na watapambana kwa kuangalia kama mchezo wa fainali.
Mkwasa amesema, japo walifungwa magoli matatu hapo mwaka jana katika mchezo wa awali uliopigwa nchini misri lakini katika mpira lolote linaweza kutokea.
Mkwasa amesema, Misri ni timu ngumu na nzuri, yenye wachezaji wakubwa na wazuri lakini mpira ni dakika 90 na kila mchezaji katika kikosi cha Stars atahakikisha anapambana ili kuweza kupata matokeo na kuwapa furaha watanzania kwa ujumla.
Kikosi cah Taifa Stars kiliingia kilitangazwa Mei 18 mwaka huu ambapo mara baada ya kumalizkamkwa msimu wa 2015/16 wa Ligi kikosi kiliingia kambini Mei 23 kikiwa na wachezaji 13 ambapo mara baada ya kumalizika pia kwa fainali za kombe la Shirikisho Tanzania Bara kati ya Azam FC na Yanga kikosi kiliingia kambini kikiwa na wachezaji 25 ambacho kilielekea nchini Kenya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Wachezaji wa Kimataifa Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu waliingia nchini wiki hii ambapo mojha kwa moja walijiunga na kikosi na kuendelea na mazoezi.