Thursday , 16th Jun , 2016

Mshambiliaji wa Simba Mussa Hassan Mgosi amesema suala la kuongeza mkataba klabu ya Simba ni mpaka pale mazungumzo baina yake na viongozi wa Simba yatakapokwenda sawa.

Mshambiliaji wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi

Mgosi amesema, mpaka sasa hana wasiwasi na maisha yake Msimbazi kwani kila kitu kinakwenda sawa.

Mgosi amesema, mazungumzo yanaendelea na mpaka sasa yamefikia pazuri na anaamini msimu ujao ataweza kuendelea kuitumikia Simba.

Kwa upande mwingine Mgosi amesema, amekuwa akipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kuwa anapaswa kuendelea kuwa Simba ili baadaye apewe mikoba ya ukocha lakini anasubiri kuona kama hayo yatawezekana.