Thursday , 2nd Feb , 2017

Misri imeweka rekodi kwa kufanikiwa kufuzu kwa mara ya tisa katika fainali za kombe la Afrika baada ya kuishinda Burkina Faso 4-3 katika mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa usiku wa kuamkia leo.

Mlinda mlango wa Misri Essam El Hadary

Kwa hatua hiyo, Misri inakuwa imeweka rekodi ya kuwa taifa pekee liliyotinga fanali mara nyingi zaidi katika michuano, huku likishikilia pia rekodi ya kuwa taifa lililoshinda mara nyingi zaidi kombe hilo, likiwa limeshinda mara 7. 

Mlinda lango wa muda mrefu Essam El Hadary alithibitisha ushujaa wake kwa kuokoa penati iliyopigwa na Betrand Traore na kuiwezesha Misri kupata ushindi huo.

Wakati wa muda wa kawaida Mohamed Salah aliiweka kifua mbele Misri baada ya kufunga bao lililosawazishwa na Aristide Bance kwa krosi iliopigwa na Charles Kabore.

Mchezo mwingine wa nusu fainali, utapigwa usiku huu, kati ya Cameroon na Ghana, na mshindi wa mchezo huo, atakutana na Misri, Jumapili Februari 5.