Friday , 18th Sep , 2015

Mikoa iliyochini ya Chama cha Mpira wa Wavu nchini TAVA imetakiwa kuanzisha mafunzo mbalimbali kwa waamuzi ili kuweza kuwa na waamuzi wengi watakaoweza kuchezesha michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa TAVA Muharame Mchume amesema, TAVA inashindwa kuandaa mafunzo mara kwa mara kwasababu inafuata kalenda ya shirikisho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya DAREVA Nassoro Sharif amesema kila mwamuzi aliyeshiriki kozi hiyo atatakiwa kuchezesha mechi sita ili aweze kupata cheti ya ngazi ya ufaulu katika awamu ya pili kwani vyeti walivyovipata hii leo ni vya ushiriki wa kozi hiyo.

Sharif amesema, washiriki wengi hushiriki kozi mbalimbali ili kuwa na vyeti ambavyo huvitumia tofauti na kama inavyokusudiwa, hivyo hivi sasa waamuzi wote watatakiwa kutumia elimu waliyoipata ili kuweza kuukuza mchezo huu hapa nchini.