Akizungumza na East Africa Radio, Masai amesema mashindano hayo hushirikisha wachezaji chipukizi na wale wa zamani ambao wapo katika viwango vya juu kimchezo ili kuweza kuleta changamoto katika mchezo huo.
Masai amesema, kwa upande wa walimu mwaka jana walikuwa na mwalimu mmoja ambaye alikuwa ni maalumu kwa ajili ya kufundisha mchezo wa Gofu lakini kwa mwaka huu wamepata mwalimu mwingine ambapo watakuwa wawili kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo huo kwa wanamichezo wa mchezo huo hapa nchini.
