"Manchester City ni moja ya timu kali zaidi duniani wakati huu sambamba na PSG wako vizuri sana kwasasa," amesema mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina.
Kwa upande mwingine Messi amesema kitendo cha Barcelona kutopoteza mchezo wa ligi hadi sasa inaonesha kuwa timu hiyo imeimarika zaidi hata baada ya kuondokewa na nyota wake Neymar Jr, aliyetimkia PSG.
"Tunauwiano mzuri zaidi bila Neymar, kuondoka kwake kulifanya tubadili namna ya kucheza japo iliathiri safu yetu ya ushambuliaji, lakini tumekuwa bora sana kwenye eneo la kiungo na ulinzi na inaturahisishia kushinda mechi'', amesema.
Barcelona kwasasa inaongoza ligi kuu nchini Hispania ikiwa na alama 54 ikifuatiwa na Ateltico Madrid yenye alama 43. Leo Barcelona itashuka dimbani kuivaa Alaves.


