Wednesday , 10th Feb , 2016

Timu ya Azam FC imesema hawatishwi na kazi ya timu yoyote shiriki ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara kwani wanaamini kwa watafika pale wanapotarajia.

Kocha Msaidizi wa Azam FC Denis Kitambi amesema, kwa sasa wanakiandaa kikosi chao kushinda kila mchezo uliopo mbele yao ikiwa ile ya viporo kwa lengo la kuipiku Simba kwa sasa wapo sawa kwa pointi lakini inashika nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa nyuma ya Yanga kwa pointi moja.

Kitambi amesema, Simba wamewafikia kwa pointi kwa kuwa hawajacheza mechi mbili, lakini baada ya kucheza hizo wanaamini hawatakuwa sawa na sisi kwani nia yao ni kuwa mabingwa msimu huu na wala si kushika nafasi ya pili.

Kitambi amesema, wana nafasi kubwa ya kuongoza ligi kwani wakishinda mechi walizozidiwa watakuwa na pointi 48 na kuwaacha Simba kwa pointi sita huku Yanga wakiipita pointi tano.