
Nahodha wa timu ya iliyopenya ambayo ni Mchenga BBall Stars, Mohamed Yusufu amesema licha ya mchezo kuwa mgumu kwa kipindi chote lakini waliweza kuwasoma wapinzani wao vizuri jambo ambalo liliwasaidia kupata ushindi huo.
"Tumeweza kutumia madhaifu ya wapinzani wetu waliyokuwa wanaonesha uwanjani kama njia ya kujipatia ushindi huu ila tunamshukuru Mungu kwa kuweza kufuzu hatua hii na kuingia nusu fainali ya michuano hii", alisema Mohamed.
Kutokana na ushindi huo Mchenga BBall Stars imeweza kujikatia tiketi ya moja kwa moja kuingia kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hii inayoendelea kurindima mchana huu kati ya Flying Dribblers dhidi ya Osterbay.
Pamoja na hayo, Mchenga team wameweza kutoa mfungaji bora Rwahabura Munyagi kwa siku ya leo 'best scorer' kwa pointi 25 huku mpinzani wake Martin Kolikoli akipata pointi 12 kutoka The Fighter
Mtanange huo uliojaa upinzani mkubwa kwa kila mmoja kutaka kupata ushindi umechezeshwa na refa Shaban Mohamed pamoja na msaidizi wake 'Empire' Edwin Kilagwa.