
Mbwana Samatta
Samatta ameyasema hayo kwenye mahojiano na kituo kimoja cha Television, ambapo ameweka wazi kuwa licha ya kupiga hatua ambayo inaonekana kuwa kubwa lakini yeye haoni kama amefika zaidi anaendelea kujituma ili siku moja aweze kuchezea vilabu vikubwa zaidi ya Genk.
''Wanasema maisha nimeyapatia kwa kiasi flani ni kweli lakini hapa nadhani nipo Genk na sio Real Madrid wala Barcelona, ndoto bado iko palepale kucheza katika vilabu vikubwa ambavyo tulikuwa tunavitazama tu'', amesema.
Samatta ambaye ameanza vizuri msimu huu kwa kufunga mabao katika timu yake kwenye ligi kuu ya Ubelgiji pamoja na Europa League ameripotiwa kuhitajiwa na vilabu kadhaa vya England ikiwemo Everton.
Nahodha huyo wa Stars kwasasa yupo nchini Cape Verde akiwa na kikosi cha Taifa Stars tayari kwa mchezo wa kundi L kuwania kufuzu AFCON 2019 utakaopigwa Oktoba 12, 2018.