Sunday , 10th Jan , 2016

Mganda, Jackson Mayanja ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa Simba SC, kufuatia kuondoka kwa Suleiman Matola miezi miwili iliyopita.

Mganda, Jackson Mayanja ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa Simba SC, kufuatia kuondoka kwa Suleiman Matola miezi miwili iliyopita.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba Mayanja aliyekuwa anaifundisha Coastal Union ya Tanga, amejiunga na kikosi hiko huko visiwani Zanzibar kuanza kazi, chini ya kocha mkuu, Muingereza, Dylan Kerr.

Manara amesema wamemchukua Mayanja kwa kuwa ana uzoefu wa ligi ya Tanzania kwa kuwa alishawahi kufundisha Kagera Sugar kwa miaka 3, na kabla ya kuja Simba alikuwa kocha wa Coastal Union ya Tanga.

Kocha huyo ambaye alishawahi kuwa kocha msaidizi wa Uganda kwa miaka 9, anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Simba SC wenye kipengele cha kuongezewa, iwapo kazi yake itawaridhisha wenye timu.