Thursday , 22nd May , 2014

Mashindano ya michezo mbalimbali kwa vyuo vikuu vya nchi za Afrika Mashariki yanatarajiwakufanyika jijini Nairobi kuanzia mwezi julai mwaka huu

Wanamichezo toka chuo kikuu cha Mkwawa wakipita kwa maandamano ya ufunguzi wa mashindano ya vyuo vikuu Afrika Mashariki mwaka 2013 yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Shirikisho la michezo ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki limesema michuano ya mwaka huu ya vyuo vikuu kwa nchi za Africa mashariki inataraji kufanyika jijini Nairobi Kenya mwezi Julai mwaka huu,

Makamu wa Rais wa shirikisho la michezo kwa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki Noel Kihunsi amesema maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao kilichofanyika hivi karibuni nchini Uganda na hivyo wao kama shirikisho kwa hapa nchini watafanya kikao kwaajili ya kupanga mikakati ya ushiriki wa vyuo vya hapa nchini

Aidha Kihuns amesema katika kuhakikisha vyuo vikuu vya Tanzania vinafanya vema wanataraji kukutana hivi karibuni wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwajili ya mkutano maalumu wakupanga mikakati juu ya ushiriki wa vyuo vyetu katika michuano hiyo mikubwa kwa vyuo vikuu kwa ukanda wa Afrika Mashariki.