
Kocha wa timu ya taifa na mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Meza nchini TTTA, Yahya Mungilwa amesema, mashindano hayo yanalenga kuhakikisha wanawapima viwango wachezaji wakongwe wa timu ya Taifa na kuibua vipaji vipya kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Mungilwa amesema, baada ya kuandaa kozi ya kimataifa ya ukocha daraja lapili inayotarajia kufanyika mwezi Julai mwaka huu watatoa mwezi mmoja ili makocha hao waweze kutumia kile walichojifunza kuwafundisha wachezaji ili waweze kucheza kisasa katika mashindano ya Taifa.
Kwa sasa TTTA haikabiliwi na mshindano yoyote ya kimataifa baada ya mwaka jana kushindwa kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa kutokana na kukabiliwa na ukata.