Thursday , 4th Dec , 2014

Mashindano ya Ngumi Taifa yameingia mzunguko wa pili leo huku baadhi ya mikoa shiriki katika mashindano hayo ikionekana kufanya vizuri.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania BFT, Wililo Lukelo amesema katika michuano hiyo wameweza kuona vipaji vingi na wanaamini watapata vipaji vingi kwa ajili ya kuunda timu ya Taifa ya Ngumi ya muda mrefu.

Lukelo amesema mikoa mbalimbali inatakiwa kujitokeza kushiriki mashindano mbalimbali ya ngumi ili kuweza kupata timu bora ya taifa itakayoweza kuiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.