Friday , 31st Oct , 2014

Bondia Thomas Mashali amesema amejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano la Middle weigth la uzito wa kilo 76 atakalopigana dhidi ya Bondia kutoka nchini Kenya Henry Wandera hapo kesho ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es salaam.

Bondia Thomas Mashali

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mashali amesema licha ya bondia huyo kuogopwa kwa kazi zake lakini anaamini atafanya vizuri zaidi ya pambano lililopita la ubingwa wa UBO lililopigwa Mkwakwani jijini Tanga.

Kwa upande wake Wandera amesema hajaja kucheza katika pambano hilo bali amekuja kupigana na anatarajia kumpiga Mashali katika raundi ya nane.