Sunday , 5th Jun , 2016

Michuano maalumu ya kombe la kuadhimisha miaka 100 ya michuano ya Copa Amerika imeanza kwa matokeo ya kustusha kwa baadhi ya timu zilizopewa nafasi ya kufanya maajabu katika michuano hiyo ya kihistoria zikianza kwa vipigo na sare katika michezo yao.

Sebastian Perez wa Colombia (kulia) akipasua katikati ya wachezaji wa Marekani.

Michuano ya Copa America iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya kusherehekea miaka 100 ya kuanziashwa kwake imeanza kwa kishindo ikishirikisha mataifa 16 kutoka katika mabara yote ya America, kusini na kaskazini.

Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya taifa kufanyika nje ya bara la Amerika ya kusini tangu kuanzishwa na kuasisiwa rasmi kwa michuano hiyo mnamo mwaka 1916 ambapo kwa sasa imebeba sura tofauti na ilivyozoeleka ikishirikisha timu za mabara tofauti ya Amerika.

Hii ni michuano ya 45 ya Copa Amerika na inafanyika kama sehemu ya maadhimisho ya na nimaafikiano baina ya mashirikisho ya kati ya CONMEBOL – Shirikisho la soka la America kusini na CONCACAF [Shirikisho la soka Amerika Kaskazini, kati na Caribian] ambayo itakuwa ikifanyika katikati ya michuano ile ya kila baada ya miaka minne ikihusisha mataifa 16 badala ya 12 ya kawaida.

Ambapo timu zote 10 kutoka CONMEBOL zinashiriki sambamba na sita kutoka CONCACAF.

Mshindi wa michuano hii maalumu hatashiriki katika kombe la mabara la FIFA mwaka 2017 kwakuwa Chile ilishafuzu kwa kushinda taji la Copa Amerika mwaka Jana.

Wakati michuano hiyo ikiwa imeanza ama kukata utepe alfajili ya kuamkia jana na kushuhudia matokeo yasiyotarajiwa kwa baadhi ya vigogo kupoteza michezo amaa kutoka sare.

Wenyeji Marekani wao walianza ufunguzi kwa kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa Colombia huku hii leo alfajili ikishuhudiwa vigogo wengine Brazil wao wakilazimishwa suluhu ya 0-0 na Equador.

Lakini ni matarajio ya mashabiki wengi kuwa ugumu wa mashindano hayo utachagizwa na vikosi vya timu zote ambavyo vinaundwa na nyota wanaocheza ligi kubwa katika nchi mbalimbali duniani kote.

Mfano wa wanaotarajiwa kuwika ni pamoja na kina Lionel Messi, wa Algentina, Luis Suarez wa Uruguay, Naymar wa Brazil, Harvie Hernandez [chicharito] wa Mexico na wengine wengi.

Michezo itakayopigwa usiku na alfajili ya kuamkia kesho ni pamoja na ule kati ya Jamaica dhidi ya Venezuela utakaochezwa milango ya 6 usiku kwa EAT nakufuatiwa na mchezo mgumu mno baina ya Mexico na Uruguay huu ukianza milango ya saa tisa alfajili