Wednesday , 6th Jan , 2016

Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mchezo wa Mpira wa Magongo unatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari nane mpaka 12 mwaka huu viwanja vya lugalo jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa chama cha mpira wa magongo nchini THA Mnonda Magani amesema, michuano hiyo itashirikisha timu takribani 10 kutoka Tanzania Bara ambazo ni Moshi Kalser, Dar es salaam Kalser, Arusha, Tanga Stars, Dar es salaam Institute, Magereza pamoja na TPDF huku Lindi na Kibasila zikitarajiwa kukamilisha zoezi la uhakiki wa ushiriki kabla ya siku ya mshindano.

Magani amesema, maandalizi kwa upande wao kama uongozi na wanaamini timu zote shiriki zitakuwa na ushindani na kuweza kupata kikosi bora cha timu ya taifa.

Mashindano hayo yana lengo la kuunga mkono maadhimisho ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.