Mlinda Mlango wa Simba sc,Manyika Peter
Akizungumza na East Africa Radio,Manyika amesema mashabiki wasitegemee makubwa sana kutoka kwake lakini anaamini kutokana na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji wenzake atazidi kufanya vizuri katika mechi mbalimbali.
Kwa upande wake mlinda mlango wa timu ya Yanga Deogratius Munish Dida amesema japo ni mara ya kwanza kwa Manyika kulinda lango la Simba anaamini kwa uwezo aliouonesha atafika mbali zaidi katika soka hapa nchini.