Wakati man United leo ikishuka dimbani kuumana na Newcastle United ugenini, Kocha wake Luis Van Gaal amekiri kuchukizwa na baadhi ya michezo ambayo timu hiyo imecheza.
Kocha huyo ambaye amekuwa na wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kiwango cha timu hiyo, amesema kuwa ingawa kuna baadhi ya michezo ameifurahia, mechi nyingi timu hiyo imecheza vibaya bila mpangilio wala malengo ya kupata ushindi.
Katika mchezo wa juzi dhidi ya Sheffield United, mashabiki wa timu hiyo waliondoka uwanjani mapema, na alipoulizwa anafikiri ni kwanini mashabiki waliondoka mapema, akajibu kuwa anadhani walifikiri timu isingeweza kufunga na pia ni kwa sababu ya kuwahi foleni za barabarani.
Van Gaal amewataka mashabiki wa timu hiyo duniani kote kuifurahia timu yao licha ya kutoonesha mchezo mzuri na kwamba ana imani ya kupata ushindi katika mchezo wa leo wa ugenini dhidi ya Newcastle.
Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni Aston Villa itakayoikaribisha Crytal Palace, na West Ham itakuwa ugenini dhidi ya Bounaermouth.

