Thursday , 28th Jan , 2016

Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Jamal Malinzi ameomba radhi kwa watanzania kwa kuiruhusu Azam FC kwenda kwenye “Bonanza” nchini Zambia, wakati ligi kuu ya soka Tanzania Bara ikiendelea.

Malinzi amesema, Malinzi amesema wakati TFF inatoa ruhusa kwa Azam FC yeye alikuwa nje ya nchi na ndio maana ameamua kuomba radhi kwa kuwa haikuwa sahihi na ndiyo maana ameamua kuwa muungwana.

Malinzi amesema, Azam FC wakirudi watakuwa kwenye kipindi kigumu kwani atalazimika kucheza mara mbili kwa wiki yaani Jumatano na Jumamosi ili wamalize mechi na kulingana na wenzao.

TFF imezua zogo na gumzo baada ya kuiruhusu Azam FC kwenda Zambia ikiwa ni baada ya kucheza mechi tatu, wakitokea mapumziko ya Kombe la Mapinduzi.

Kwa upande wa Katibu Mkuu TFF, Mwesigwa Celestine hapo jana alionekana kujichanganya baada ya kusema bodi ya ligi walisema hawana shida Azam FC kuruhusiwa kwenye kushiriki bonanza la Zambia huku Bodi ya ligi nao wakisisitiza kwamba Azam waliomba ruhusa muda mwingi.