
Kikao hicho kilichokuwa na washiriki toka pande zote za mgogoro ambao ulipelekea mambo ya mpira kupelekwa mahakamani waliafikiana uitishwe mkutano mkuu kwa upande wa shirikisho la soka Zanzibar (ZFA) wa dharura kuweza kujadili mwenendo wa kamati ya utendaji ikiwemo kuandika katiba mpya ya shirikisho hilo.
Katika kikao hicho, imeafikiwa kuwa, Rais wa ZFA Ravia Idarus kwa mujibu wa katiba ya ZFA ndiye atakeyeitisha mkutano huo huku Kamati ya sasa inayoendesha ligi Zanzibar ikiongezewa wajumbe watatu watakoteuliwa na Rais wa ZFA pamoja na kuteua kamati ndogo ya kuandika upya Katiba ya ZFA.
Katika kikao hicho cha usuluhishi, wote waliohusika kupeleka masuala ya soka mahakamani wamekubali kuyaondoa.