Friday , 18th Apr , 2014

Wachezaji wa soka walio na umri chini ya miaka 17 kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam nchini Tanzania Jumatatu ya April 21 mwaka huu kushiri katika mafunzo ya siku tano ya mpango wa kukuza vipaji kwa vijana .

Wachezaji wa timu ya wanawake wakichuana katika moja ya mashindano hayo

Wachezaji wa soka walio na umri chini ya miaka 17 kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam nchini Tanzania Jumatatu ya April 21 mwaka huu kushiri katika mafunzo ya siku tano ya mpango wa kukuza vipaji kwa vijana unaojulikana kama Airtel Rising Star.

Akitangaza ujio wa vijana hao, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando amesema hiyo ni fursa kwa vijana wa kitanzania kuonesha uwezo wao ambapo mafunzo hayo yatafanyika katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania Jamal Malinzi amesema mpango huo una umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya soka kwa vijana wadogo ambao ndio chimbuko la maendeleo ya mpira wa miguu nchini.