
Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF Saleh Zonga amesema mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha timu mbalimbali kutoka katika mikoa ambao ni wanachama wa TBF.
Zonga amesema, kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, mwishoni mwa mwaka huu watakuwa na kozi kwa makocha katika kila mkoa wanachama wa mchezo huo ili kuweza kukuza zaidi mchezo huo ambao umeonekana kushuka hadhi yake kutokana na kukosa wadhamini tofauti na ilivyo kwa upande wa soka.
Zonga amesema, katika mipango yao wanatarajia kuandaa mashindano ya vijana kwa lengo la kuunda timu ya taifa itakayoshiriki michuano ya kitaifa na kimataifa.